Jumatatu, 27 Februari 2017

Stella Mollel: Kwanini naishiwa sauti wakati wa mazoezi ya uimbaji?

Haleluya mtu wa Mungu popote pale ulipo!
napenda tushirikiane swali hili lililoulizwa na dada Stela Mollel kwamba: 
"KWANINI NAISHIWA SAUTI WAKATI WA MAZOEZI YA UIMBAJI/uimbaji?"
Yamkini,Stella amewakilisha tu watu wengine wenye tatizo kama hili la kupungukiwa sauti au kukauka sauti wakati wa uimbaji. Swali hili limeulizwa katika darasa linaloendelea la HOW TO SING BETTER pamoja na mtandao huu kwa msaada tu wa Mwenyenzi Mungu. 
  Ninayo neema ya kuweza kulijibu swali hili kama ifuatavyo.
Kuna kitabu kimoja kinaitwa MUSIC PRACTICE AND THEORY(unaweza kukitafuta) kimethibisha kwamba waimbaji wengi kati yao wanapungukiwa sauti kwa sababu mbali mbali. Lakini sababu moja kuu ni: MWIMBAJI KUTOPATA MUDA  WA KUTOSHA KUPUMZIKA. kwa kimombo twaweza kusema lack of enough time for resting. Katika hili tunaweza kuona kwamba waimbaji wengi tunafanya sana matamasha nyakati za usiku (sio mbaya). Ubaya unapokuja ni pale ambapo mwimbaji anatumia muda mwingi (24/7) kufanya zoezi la uimbaji akiamini kwamba anajinoa vyema. ni kweli ni muhimu kujinoa lakini kumbe unatakiwa utenge muda wa kutosha kupumzika/kulala kabla ya kwenda kuperform(kuimba).
  Ieleweke kwamba ikiwa utakua na muda mchache wa kupumzika /kulala (less than 8hrs), ukakosa na maji ya kunywa kwa wingi (hydration) na huku unatarajia uimbe kwa muda mrefu na mahali pengi tena kwa masaa au siku kadhaa basi tutegemee badiliko lolote hasi kwenye sauti yako ya kuhudumia (kuimbia).
    Kwa bahati nzuri nimepata neema ya kuwa "linked" na taaluma ya afya ya binadamu, Hivyo kwa ushauri wa kitaalamu pindi unapokua umepatwa na tatizo la kupungukiwa na sauti au kukauka kwa sauti  kabisa wakati wa kuimba, chukua hatua ya kuacha kuimba kwa muda, yaweza ikawa kwa masaa, siku, wiki au mwezi kutegemeana na ukubwa wa tatizo lako lenyewe ulilonalo. 
    HITIMISHO
 Ukihisi una tatzo la upungufu wa sauti au sauti kukauka, pata muda wa mapumziko na kisha kunywa maji ya kutosha ili kulainisha "vocal cord" 


MUNGU AKUBARIKI SANA.

Ev Mhugo Hantish (the sound of worship)
TANGAZO!!
KAMA KUNA MTU ANAPENDA KUJIUNGA NA DARASA LA UIMBAJI BORA AWASILIANE NASI KWA NAMBA 0768788303 AU ATUME BARUA PEPE KWENDA hantishmhugo@gmail.com.
usisahau pia kutembelea blog yetu hii hapa chini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni