HOW TO SING BETTER CLASSROOM
With Ev Mhugo Hantish
Kama utakua na swali lolote uliza kwa namba
0768788303.
…………………………..
FAHAMU
NINI MAANA KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA
Nini maana ya kusifu na kuabudu
KUSIFU NA KUABUDU ni maneno
tofauti na yana maana tofauti
1. kusifu
MAANA --- nikuelezea wasifu au
wajihi za kitu au mtu. Sasa tunaposema tunamsifu Mungu inamaanisha ni KWA
KUMUINUA JUU, KUSHUKURU KUMPAZIA SAUTI,KUFANYIA SWANGWE, KUJISHUSHA CHINI YAKE
KWA UNYEYEKEVU,nk Zaburi 100:4
Neno hili kusifu kwa kiebrania
lilikuwa na maana ya;
Tehila, yaani kutamka neno kwa
kuongeza vionjo na mbwembwe zaidi. Mfano neno haleluya unalitamka (Ha, ha
leluya huuu eee) Tehila ni kuwa kama kichaa unaposifu au kuabudu kwa utukufu wa
Bwana. (Nilidhani labda hapa ndipo waswahili walipopata neno taahila).
Yadaa yaani kujiachia kwa Mungu
(you just surrender yourself to the Lord).
Barak yaani kusaluti mbele za
Bwana. Ni kuonyesha kwamba ni yeye peke yake anayestahili heshima na utukufu.
Huwezi kumpigia saluti mtu usiyemwona, hivyo ni kwa njia ya kumwabudu Mungu
katika roho na kweli ndipo tunapomwona kama alivyo na utukufu wake
2. Kuabudu
Neno la Kiebrania shachah lina
maana ya kuabudu, kusujudia, kuinama kwa kuonesha unyenyekevu, kuonesha heshima
kubwa au kuanguka kifudifudi. Neno la Agano la Kale proskuneo halikadhalika
lina maana ya kubusu mkono, au kupiga magoti na kugusa ardhi kwa paji la uso
kwa unyenyekevu mkuu. Maneno mengine mawili ya kuabudu yana maana ya kutumika,
kufanya ibada Takatifu na kumtolea Mungu Sadaka.
Waache Watu Wangu Waondoke, Ili
Wapate Kunitumikia, Dai hili Mungu alilolirudia mara kwa mara lilipelekea Farao
kuwaruhusu watu wa Mungu kutoka Misri. Tangu wakati huo, Mungu, Mungu mwenye
wivu, amekuwa akipambana na watu wake akiwazuilia kuabudu miungu mingine na
sanamu, na badala yake wamwabudu Mungu aliye hai na wa kweli. Kutoka 7:16
Ibada ni kumtukuza Mungu na
kumfurahia daima. Mungu anawatafuta watu wa kumwabudu, na kufanya ibada ndiyo
wito wetu wa kwanza (Yn4:23 Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo
halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio
Baba anawatafuta. Msitari wa 24 unasema Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu
imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.). Ibada ya kweli ni pale
tunapomruhusu Roho Mtakatifu atuongoze kutoka katika roho zetu au mioyo yetu
kuabudu katika roho na katika kweli na sio tumaini letu ktk miiliau akili zetu
Flp 3:3.
Ibada ni tendo la thamani kubwa,
ni la kipekee na linamhusu Mungu (utatu mtakatifu) ambao peke yao wanastahili.
Lucifer, aliyekuwa mhusika mkuu wa ibada huko mbinguni, alitaka ibada hiyo iwe
kwa ajili yake, maana yake aabudiwe yeye badala ya Mungu; na hilo ndilo
lililopelekea kuanguka kwake (Isaya 14 na Ezekieli 28). Hata wakati fulani
alitaka Yesu amsujudie ili eti ampe falme zote za dunia lakini Bwana alikataa
Mt4:8-10.
Kwa hiyo kuabudu ni ibada na
tunaposema ibada sio zile taratibu za kibinadamu tulizojipangia katika ibada
zetu za siku za leo, ibada za leo tumeweka mambo mengi sana na yanatumia muda
mwingi sana kuliko ile maana hasa ambayo mungu aliikusudia katika agano la kale
utana ibada zilikuwa zinafaywa kwa mambo makuu 2 neno la Mungu, na Kuabudu.
Kuabudu ni sehemu ya maisha
wanadamu tumeumbiwa kuabudu, watuwezi kuishi bila kuabudu hapa haijalishi
unaabudu nini!!! Unaweza kuwa unaabudu Mungu wa kweli au miungu kama ambavyo
ukisoma bilia utaona kuna miungu mingi inatajwa mfano Baali, Dagon ink na hata
leo iko miungu mingi ambayo wanadamu wanaiabudu lakini wa kuabudiwa ni mmoja
tu. Na katika biblia tunaona kuaudu kwa mara ya kwanza kulikofanywa na Ibrahimu
kutoka katika kitabu cha mwanzo 12: 8 Psalms 34:1 inaonyesha tunatakiwa
kumwabudu Mungu kila wakati.
Kwanini tuabudu
kuabudu ni agizo kutoka kwa Mungu
kutoka 20 2-4 . Psalm 96:9, Psalm 29:2 Tunapomwabudu mungu naye Mungu
hufurahiwa na sisi Zephaniah 3:17 Rom 12:1-2
Your Worship = Your View of God
jinsi unavyoabudu ndiyo mwonekano
wa mungu ulivyo ndani yako, haijarishi unaabudu wapi uwe peke yako au mko wengi
kama unaabudu kwa kutokumaanisha au kumaanisha itajulikana tu na hivyo ndivyo
mtu anaweza kujua ni jinsi gani mtazamo wako kwa Mungu wako.
KUNA NGUVU KATIKA KUSIFU NA KUABUDU
Yoshua 6:20 Matendo 16:23-26
zinaonyesha ambavyo kwa kutumia kusifu tu Mungu alishuka na kufanya lile
lililokuwa hitaji lao.
Kusifu kunamfukuza adui
Psalms 50:23. 2 Nyak 20:22. Ukiwa
unasifu na kuabudu humfukuza adui mbali kutokana na ukiwa kwenye ibada Mungu
hushuka maana yeye anasema anakaa katikati ya sifa hivyo palipo na Mungu
shetani hawezi kuwepo lazima akae mbali.akimbie mbali kabisa maana kunakuwepo
na uwepo wa bwana wa Majeshi.
Je, ni wakati gani tuabudu?
Ni niyakati zote zinafaa
kumwabudu Mungu. Kwa nyakati zilizotengwa Zaburi ya 100 inatuelekeza namna ya
kuanza, lakini zaidi ya yote tunapaswa kuishi maisha ya ibada bila kukoma. Kwa
kila tunapopumua, kwa kila wazo, kwa neno na tendo, tunapaswa kumwabudu Mungu
wetu mzuri tunayemtumikia milele na milele Zab 145:1,2
mwa 12:6- Siku zilipita na watu
wakafanyia ibada kwenye Hekalu na kwenye masinagogi; lakini siku hizi miili
yetu ni hekalu la Mungu 1Kor 6:19 tu hekalu la Mungu sisi ibada zinatakiwa
zifanyike kila wakati na si mara moja kwa wiki kama wengine wanavyo dhani.
Je, Tunafanyaje Ibada?
Biblia inatufahamisha jinsi watu
walivyotumia mioyo yao, mawazo yao, mikono yao, viganja vyao, miguu yao, na
midomo yao katika uimbaji. Walipaza sauti zao kwa furaha na kusujudu, kucheza,
kusifu, kubariki na kushukuru.
Maneno kama halal na haleluya
kutoka katika Zaburi yana maana ya kusifu, kumwinua na kumwadhimisha Bwana.
Neno Yadah lina maana ya kunyoosha mikono hewani, na neno barak lina maana ya
kupiga magoti katika ibada ya kumbariki Mungu. Kuitoa miili yetu katika
kumhudumia Mungu na mwanadamu ni ibada pia (Rum 12:1). Watu pia humwabudu Mungu
katika sanaa zao, katika uandishi wao, katika michezo ya kuigiza, katika
muziki, katika usanifu wa majengo, na hata katika utoaji wa fedha zao kwa ajili
ya Injili.
Kusifu na kuabudu sio kuimba tu
Watu wengi wanajua kuwa kusifu na
kuabudu ni kuimba tu hapana kuna njia nyingi za kusifu au kuabudu, unaweza
kutumia sanaa nyingine kumwabudu mungu au watu wengine wakamwabudu Mungu mf
maigizo, ngonjera, shaili, uchoraji, upambaji au unakshi wa vitu, kujenga .nk
Ibada Kanisani
KatIka kanisa makusanyiko yetu
yanapaswa kujawa na zaburi, nyimbo, na tenzi za rohoni ambazo zinaweza
kuongozwa na Roho katika lugha mpya anazotupatia Yeye. Kwahiyo mikutano mingi
ya kisasa haina tofauti sana na burudani za kikristo kama kwenye kumbi za
starehe. Watu huwa wanaangalia tu, lakini je, wanaabudu? Uwepo wa Mungu na Roho
wake katika ibada zetu utawafanya watu wasioamini kuanguka chini na kuabudu
(Kol 3:16) (1Kor 14:15,16,25,26) (Efe 5:19) (Mdo 2:4).
Ibada Ya Kweli Ina Gharama
Biblia inazungumzia habari za
sadaka za kusifu. Daudi alicheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote, na
akakataa kumtolea Mungu kafara ambayo isingemgharimu cho chote (2Sam 6:14;
24:24). Wale mamajusi wa Mashariki walitoa zawadi za gharama kubwa walipokuja
kumwabudu Yesu (Mt 2:9-12), na mwanamke mmoja alimpaka Yesu kwa mafuta ya
gharama kubwa, akamwosha miguu yake kwa machozi yake, na kuifuta kwa nywele
zake (Lk 7:36-50). Hivyo ibada yoyote inaambatana na kutoa tena vitu vyetu vya
thamani.
Tunapaswa kumsifu Mungu kwa jinsi
alivyo na kwa matendo yake; lakini Mungu mwenyewe anawatafuta na anawataka
wafanya ibada, na si mradi ibada tu. Kusifu kwaweza kufanywa hadharani, lakini
ibada mara zote ni jambo la ndani ya moyo. Kusifu mara zote kunaweza kuonekana
au kusikika, lakini kuabudu yaweza kuwa ya kimyakimya na iliyofichika. Kusifu
kunaonekana, kuna kutumia nguvu, kuna misisimko na furaha; lakini ibada mara
zote ni heshima na hofu katika uwepo wa Mungu.
Biblia pekee inatuonesha jinsi
Mungu anavyo hitaji na kutamani kuabudiwa na yeye pekee yake ndiyo anayestahili
kuabudiwa.
Kusifu na kuabudu kwa siku za leo.
Katika siku za leo kuna ufinyu wa
mafundisho katika kusifu na kuabudu na ndiyo maana ya kuanda somo hili ili
tupanuane mawazo. Watu wengi wa leo wanadhani kusifu ni kuimba kwa nyimbo zenye
midundo ya harakaharaka(zouk&sebene) na ukipunguza spidi ndo kuabudu. Hasha
tunaposema kusifu inatokana na maneno yaliyopon kwenye wimbo husika kweli ni ya
kusifu, kama ni maneno ya kusifu tunasema ni wimbo wa sifa haijarishi speed
inayotumika na hali kadhalika nyimbo za kuabudu. Watu katika kipengele hiki
huwa wanachakanya nyimbo utakuta wakati wa kusifu anaimba wimbo wa kutia moyo
au wa maombi, kinachotakiwa ni kujua kuwa kila jambo lina wakati wake ziiko
nyimbo za mazishi, kufariji, kutia moyo, za maombi, za kusifu , na za kuabudu
nk sasa usichanganye kwenye kusifu wewe unaimba parapanda italia au tuonane
paradiso, hizo sio za sifa sasa najua wewe utafanya zoezi la nyimbo unazozijua
ili kufahamu zina ujumbe gani na ziko katika kundi lipi kati ya hayo
niliyokufundisha hapo juu.
Baadhi ya maandiko yanayo onyesha aina za
kusifu na kuabudu kwa:
1. Kusimama (Zab 135:1-2, 134:1)
2. Kuinua mikono (Zab 134:2,
28:2)
3. Kuinama au kupiga magoti (Zab
95:6)
4. Kupiga makofi (Zab 7:1)
5. Kucheza (Zab 149:3, 150:4,
2Sam 6:14)
6. Kicheko (Zab 126:2, Ayu
8:20-21)
7. Kufurahi (Kumb 12:11-12, Law
23:40)
8. Kutembea (2Nya 20:21-22)
9. Shangwe (Zab 95:1)
10. Kupiga kelele (Zab 66:1, Law
9:23-24)
11. Kupiga vigelegele (Zab 33:1,
32:11)
12. Ukimya (Mhu 3:7)
13. Kupaza sauti (Isaya 12: 6,
Zab 42:4)
14. Kulia/ kutoa machozi katika
roho mtakatifu
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza
ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Ev Mhugo Hantish
(the sound of worship)