Jumatatu, 6 Machi 2017

TOFAUTI YA MUZIKI NA NYIMBO

                    
         Na Ev Mhugo Hantish (the sound of worship)

   Shalom mtu wa Mungu popote pale ulipo 🎼🌍🌐
 Natumaini wote tuhai na afya njema. Kama laah basi yote yapaswa kushukuriwa kwa Mungu.

Jana tuliulizwa swali kwamba TUNAWEZAJE KUTOFAUTISHA KATI YA SENTENSI HIZI MBILI: KUUSIKILIZA MUZIKI NA KUUSIKILIZA WIMBO.
   🎶KUUSIKILIZA MUZIKI
Kwanza neno MUZIKI ni nini?
MUZIKI ni mkusanyiko wa sauti za Ala mbalimbali km Gita, kinanda, trumpet, marimba nk, au sauti zenye mfumo mzuri unaofanana na Ala za muziki. 
SIFA ZA MUZIKI
 🎶pitch
🎶Rhythm
🎶dynamics
🎶ubora wa mlio
ZIPO AINA ZA MUZIKI
🎼classic music
🎼baroque
🎼classical periods
🎼Romantic
🎼modern
🎼Opera
🎼ballet
🎼Jazz
🎼Popular music na
🎼folk music. 
Tutaendelea kujifunza kwa undani zaidi.
Lakini niseme kidogo kwamba hadi hapo kumbe huwa tunakosea kusema MUZIKI WA INJILI. hakuna muziki wa injili ila Kuna nyimbo za injili ambazo muziki wake upo kati ya aina hizo hapo juu.

NYIMBO AU WIMBO NI NINI? Ni mkusanyiko wa mashairi, tenzi, ngonjera au maneno kwa ujumla yenye MPANGILIO unaoimbika. Kuimbika huku kunaweza kusaidiwa na muziki au kusisaidiwe na muziki. (kama @Boanerge  alivyoelezea mwanzo.
Kwa maana nyingine tunaweza kusema ni kipande kifupi cha muziki wenye kuambatana na maneno ambayo huimbwa. Nyimbo hizo zinaweza kuimbwa kwa kutumia aina mbali mbali za muziki (tulizo zitaja hapo juu.)
SIFA ZA WIMBO
📀mkusanyiko wa maneno ya mashairi au tenzi au ngonjera
📀melody
📀rhythm
AINA ZA NYIMBO
📼Gospel song
📼Classical song
📼Rock song
📼County song
📼Love song
📼Ballads song
📼Metal song
📼Hip Hop song
📼Dance song
(Tutaendelea kujifunza kwa undani zaidi)

KUMBE! 💌
KUUSIKILIZA MUZIKI NI KUSIKILIZA MKUSANYIKO WA MAPIGO YA ALA YENYE MPANGILIO. MAPIGO HAYO YANAWEZA KUAMBATANA NA MANENO AU LA.

KUUSIKILIZA WIMBO NI KUSIKILIZA MKUSANYIKO WA MANENO YALIYOPANGWA KWA MTINDO WA NGONJERA AU SHAIRI AU TENZI AMBAYO YANAWEZA KUIMBIKA VIZURI.

nakukaribisha kuitembelea evhantish.blogspot.com, Mshirikishe na mwingine. Karibu kwa mchango wa mawazo yako.

Tutaendelea tena kwa wakati mwingine utakao ruhusu.

Mungu wangu akubariki.

hantishmhugo@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni