HOW TO SING BETTER?
CLASSROOM
NA MWL, EV. MHUGO HANTISH (The sound of worship)
Tel number +255768788303
Email hantishmhugo@gmail.com
Mada: Jinsi ya kuandaa wimbo.
Nafahamu kwamba wengi waimbaji kama sio wote tuna
mbinu mbalimbali za kuandaa, kuandika nyimbo. Wapo wanaoandaliwa na Roho
mtakatifu kwa njia ya maono na ndoto, wapo ambao wenyewe hutumia mapigo Fulani ya
ngoma au muziki uliandaliwa, wapo ambao wengine hukaa sehemu tulivu na salama
kwa muda kidogo. Nk.
Sasa mie leo nakuletea mada hii jinsi ya kuandaa wimbo
wako kiufasaha kabisa.
TAZAMA HAPA CHINI…
Pata wazo la liujumla, la mada unayotaka au ujumbe
unaotaka uuimbe. Kisha uhifadhi katika maarifa ambapo itakusaidia kujipambanua
zaidi. Njia hii inakupa wepesi wa kuielewa mada au ujumbe wa wimbo unaotaka
kuuandika.
upende ujumbe wako au mada yako
unayoiandaa ili ikupe fursa ya kuijadili zaidi. Kumbuka ya kwamba wewe ni kioo
cha jamii, wewe ni mhubiri, wewe ni barua inayotakiwa kusomeka kwa watu
wasioamini ili wapate kuamini. Hivyo unatakiwa kuielewa vyema mada au ujumbe
unaotaka kusema au kuuhubiri.
Baada ya kuuelewa ujumbe kisha uandike kwa
ufasaha na kwa umakini kabla ya uimbaji au melody yake kuandaliwa.
tathimini na ulinganishe ujumbe wa
wimbo uliopo na wimbo uliouandika mwenyewe kala ujautungia melody na kuuimba. Kuna
waibaji ukisikiliza wimbo wake alivyoimba labda kaimba mambo ya UPENDO WA YESU lakini
alivyouita, kaita jina la MIUJIZA YA
YESU.
soma sa na pitia sana Biblia kwa msaada wa Roho mtakatifu ili aweze
kukusaidia kupata link zinayofanana
kwenye ujumbe wako.
HUwa
inaapendeza sana zaidi pale ambapo unaweza kuzipangilizia verses zako
au kama nkwa mtindo wa mashairi ili kuepuka kurudia rudia maneno kama
mtu aliye ishiwa maneno (mistari kwa lugha ya kawaida). s
Si utakua umeshaumaliza sasa
kuuandikia wimbo kwenye ujumbe ule. Hakikisha sasa kwa hatua ya mwisho halafu
tayari kwa kuuimba acapella kwanza (inashauriwa kuimba bila beat ili ujipime
kwanza mwenyewe kabla ya kuhitaji kusaidiwa na vyombo vya muziki.)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni