Jumamosi, 4 Machi 2017

Tussah Massesse: Ni jinsi gani ya kuweza kuimba mubashara (live) bila kujichosha?

Bwana Yesu asifiwe mtu wa Mungu popote pale ulipo.
Leo tena tumepata Fursa ya kuwa ndani ya darasa la muziki na uimbaji wa nyimbo za injili.
miongoni mwa maswali yaliyojitokeza ni pamoja na swali lililoulizwa na Tussah Massesse 
kwamba:-
   "NI JINSI GANI YA KUWEZA KUIMBA LIVE BILA KUJICHOSHA?"
Anajibu  @prettymathery. anaanza kwa kusema kwamba
"ubarikiwe mtumishi wa Bwana kwa swali lako zuri, kwanza kabisa cha kufanya EPUKA KUTUMIA NGUVU KUTOA SAUTI WAKATI WA KUIMBA, maana ukitumia nguvu itakuchosha mapema. Jifunze kuimba kwa ustaarabu bila kujichosha wala kupayuka.
Pia tambua unapoimba live upo mbele ya watu. Hivyo unapaswa kuondoa woga, woga ni chanzo cha kuikausha sauti. Hivyo unashauriwa ku"Relax". Stahimili kuwa na roho ya kujiamini. Tambua ya kuwa ukipoteza tu Confidence basi ujiandae na kupotelewa na sauti au kuhama ufunguo ama kupoteza mwelekeo wa wimbo mzima".

  MAJIBU YA NYONGEZA KUTOKA KWA EV. MHUGO HANTISH
Kwa kukazia.
  Kwanza kabisa FAHAMU utatumia Muda gani katika stand up singing yako. Na pia unaimba kwa watu gani. 
 Kwanini kuhusu Muda? Itakusaidia kujipsychotherapy na kuhakikisha unaumudu Muda uliojipangia kulingana na uzoefu wako. Na ndio maana wapo waimbaji wanaoandaa matamasha ya majina yao lakini wanalazimika kuwaalika wengine ili kujipunguzia Muda ambao kwao ungewachosha.
 Kwanini Kuna umuhimu wa kufaham ni akina nani nawaimbia.?  Kwangu mie nauona umuhimu huu kwani Kuna waimbaji wamezoea kuimba kanisani kwao tu. Na huko ndiko wameshajizoelea watu wao. Lakin inapofikia hatua ya kuimba kama tamasha la kusifu na kuabudu.. Ndipo hapo tatizo linaweza kuibuka kwani mwimbaji hajawazoea watu wapya, hajayazoea mazingira na stage mpya, so kila kitu kwake ni kipya. Na ndio hapo tunaposema CHUKULIANA NA MAZINGIRA ULIYONAYO.
 Hii itakupelekea kuondoa hofu kama alivyoeleza @prettymathery. Maana hofu huua sauti kabisa.
 KIKUBWA KULIKO VYOTE MWOMBE SANA MUNGU AKUTIE NGUVU KABLA YA KUANZA HUDUMA YAKO. 
BY EV MHUGO HANTISH    

!!TANGAZO!!

1. IKIWA UNGEPENDA KUJIFUNZA KUPIGA KINANDA KWA UFASAHA KABISA WASILIANA NASI KWA NAMBA
+255768788303 
ENDELEA KUTUFUATILIA.
Tembelea pia blog yetu ya  Ev. Mhugo Hantish the sound of worship
kwa kubofya hapa  www.hantishmhugo.blogspot.com
ASANTE NA UBARIKIWE SANA.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni